Ikiwa ni tarehe 14 oktoba. 2024 siku ya kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambara Nyerere watarajali kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wametumia siku hii kwa kutembelea na kutoa zawadi mbalimbali wodi ya watoto Wachanga katika kitengo cha wazazi Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Akiongea baada ya kukabidhi zawadi Kiongozi wa Watarajali Hospitalini hapa Dkt. George Andrew amesema wameona katika siku hii ya leo watumie nafasi ya kumuenzi baba wa taifa kwa kutembelea na kutoa zawadi hizo katika wodi hizo za watoto wachanga hospitalini hapa kwa lengo la kuwashika mkono na kuwatia moyo wagonjwa.
“…tumeona tutumie siku hii ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa kuwatembelea wagonjwa na kuwatia moyo katika wodi hii ya watoto wachanga.” – Dkt. George Andrew