Wadau wa macho mkoani Mbeya leo tarehe 24, septemba, 2025 wamekutana kujadili masuala mbalimbali yahayohusu matibabu ya macho kwa watoto katika kikao kazi ikiwemo upatakanaji wa njia mbalimbali za kuwapata watoto wenye matatizo ya macho na kupatiwa matibabu kwa wakati.


Akifungua kikao hicho Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameishukuru Wizara ya Afya pamoja na wadau wa macho Nyanda za Juu kusini na kuahidi kuongeza ushirikiano zaidi endapo wataalamu watahitaji kufanikisha shughuli mbalimbali zinazohusiana na matibabu ya macho kwa watoto kupitia kambi mbalimbali za matibabu ya macho zinazoendelea katika mikoa hiyo ya Nyanda za Juu Kusini.
"sisi Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya muda wowote tuko tayari kufanya kazi mahali popote ndani ya Kanda yetu kwa kushirikiana kuhakikisha huyu mtoto anapata hii huduma pasipo kikwazo chochote." Dkt. Mbwanji
Kwa upande wake meneja wa mpango wa taifa huduma za macho Wizara ya Afya \par
Dkt. Benadetha Shiliyo amesema Tanzania imepiga hatua katika huduma za matibabu ya macho kwa watoto kwani kulinga na shirika la afya duniani kila wananchi Mil 10 kunatakiwa kuwa na kituo cha huduma za kibobezi za macho, ambapo kwa Tanzania kwa sasa kuna vituo vitano kwaajili ya huduma hiyo ikiwemo Hospitali za KCMC, Bugando, Benjamin Mkapa, CCBRT na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya


Barnabasi Mshangira ni Daktari Bingwa Mbobezi wa macho kwa watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema kuna matatizo mbalimbali ya macho kwa watoto yakiwemo yanayotibika na yanayozuilika ambapo kwa matatizo yanayotibika ni muhimu mtoto kutibiwa kabla ya miezi sabana endapo atafanyiwa matibabu baada ya hapo uwezo wa mtoto kuona huwa ni mdogo.
"matatizo ya macho kwa watoto yapo ambayo asilimia kubwa yanatibika na yapo ambayo yanazuilika." Dkt. Mshangira