SW | EN
SW | EN
Nembo ya JMT
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Afya
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya
Nembo ya HRMM

TIMU YA TIBA UTALII HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YAKABIDHI TUZO YA MSHINDI WA PILI NA CHETI CHA USHIRIKI MAONESHO YA 97 YA KILIMO NA BIASHARA ZAMBIA 2025

Timu ya Tiba Utalii inayoundwa na wataalamu mbalimbali wa afya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo tarehe 30 septemba, 2025 imekabidhi Tuzo ya ushindi na cheti cha ushiriki cha Maonesho ya 97 ya Kilimo na Biashara yaliyofanyika Lusaka nchini Zambia Agosti mwaka huu.

Akiongea wakati wa kuwasilisha ripoti na kukabidhi Tuzo ya ushindi na Cheti cha ushiriki wa maonesho hayo ofisi ya Mkurugenzi leo tarehe 30 septemba,2025 mwenyekiti wa timu ya Tiba Utalii Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Razaro Mboma amesema mwitikio ulikuwa mzuri kwani wananchi na viongozi mbalimbali walijitokeza kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kongo, Namibia na watanzania wanaosihi nchi za nje kujionea huduma hizo na hivyo kupelekea nchi ya Tanzania kuwa mshindi wa pili kati ya nchi 25 zilizoshiriki.

Akipokea Tuzo ya Ushindi na Cheti cha Ushiriki wa maonesho hayo ofisini kwakwe, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove mbwanji ameipongeza timu hiyo ya Tiba Utalii kwa jitihada kubwa zinazofanywa katika kutangaza huduma pamoja na kuiataka timu hiyo kujiwekea mikakati ya muda mfupi na mrefu ili kutangaza zaidi huduma zinazopatikana hospitali hapa pamoja na kuongeza ushirikianao na hospitalini nyingine kwa lengo la kujengeana uwezo wa kitaalamu na hivyo kuweza kusogeza huduma kwa wananchi ikiwemo nchi za jirani na hivyo kuwapunguzia wananchi gharama kubwa za kusafiri umbali mrefu.

Maonesho hayo ya ya 97 ya Kilimo na Biashara kwa mwaka 2025 nchini zambia yalianza mnamo tarehe 30 Julai,2025 na kuhitimishwa tarehe 4 agosti,2025 yakihusisha nchi 25 shiriki kutoka afrika na Tanzania kuibuka mshindi wa pili katika nchi 25 shiriki mgeni Rasmi akiwa Rais wa Botswana Mhe. Duma Boko.