SW | EN
SW | EN
Nembo ya JMT
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Afya
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya
Nembo ya HRMM

WATUMISHI WA AFYA IDARA YA WATOTO HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA WAPATIWA ELIMU KUHUSU AFYA YA AKILI NA MAGONJWA YA AKILI

Katika jitihada za kukumbushana na kujengeana uwezo kwa watumishi wa Afya kuhusu ya masuala mbalimbali, leo tarehe 26 septemba,2025 wataalamu wa Afya ya Akili na Magonjwa ya Akili wamekutana na watumishi wa afya idara ya watoto Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa lengo la kuwakumbusha kwa kuwapatia elimu mbalimbali juu ya Afya ya Akili na Magonjwa ya Akili.

Awali wakiongea ofisini kwao Dkt. Stephano Mkalilwa Daktari Bingwa wa Afya ya Akili na Magonjwa ya Akili pamoja na Betuna Mwamboneke mwanasaikolijia wote kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wamesema, lengo kubwa la kuwakumbusha watumishi kuhusu Afya ya Akili na magonjwa ya akili ni ukweli kuwa kundi la watumishi ni miongoni mwa watu wenye kundi kubwa la watu linalowazunguka nyuma yao na hivyo kupitia kundi hili itawezesha elimu hii kuwafikia watu wengi katika jamii. 

Miongoni mwa mada zilizozungumzwa ni pamoja na maana halisi ya Afya na Magonjwa ya Aakili, Vyanzo vya magonjwa ya akili, mitazamo ya jamii kuhusu vyazo vya magonjwa ya akili, aina na dalili za magonjwa ya akili, tiba pamoja mahali ambapo mgonjwa wa akili anaweza patiwa msaada.